This is a sticky topic.
X
X
 • Filter
 • Time
 • Show
Clear All
new posts

 • started a topic UNACHOTAKIWA KUJUA KUHUSU SPARK 2

  UNACHOTAKIWA KUJUA KUHUSU SPARK 2

  Tecno inafanya vizuri sana kwenye soko la ‘smartphone’ Tanzania. Hii inajidhihirisha kutokana na jinsi simu ya Spark ilivyofanya vyema mwaka jana. Mwaka huu Tecno wamekuja na Spark 2 ambayo imeboreshwa zaidi maalum kabisa kwa ajili yako wewe.

  Imekuja na umbo jembamba pia ni nyepesi yenye nchi 6.0 HD+ na wigo mpana wa kioo chenye uwiano wa 18:9 kwa kuweza kuona vizuri zaidi na kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja kwenye skrini yako.
  Click image for larger version

Name:	PICHA.jpg
Views:	1
Size:	140.1 KB
ID:	16503


  Kamera ya Spark 2 ni ‘megapixel’ 13 nyuma ikisindikizwa na flash tatu zilizokaa pamoja sehemu moja na ‘megapixel’ 8 mbele yenye flash mbili zilizokaa pamoja. Hivi vionjo vyote vinafanya kazi kwa pamoja ikiwa ni kung’aza picha na kupiga picha yenye uhalisia hata katika mwanga hafifu.

  Uwezo wa ‘Portrait mode’ umeongezwa kwenye kamera ya mbele ili pale unapopiga selfie yako, sura yako inakua inaonekana vizuri kabisa. Pia kwa mfumo wa mixed flash 2.0, mwanga wa flash ya mbele umeongezwa kwa 40% na ule wa flash ya nyuma kwa 70%.

  Spark 2 ina aina mpya ya ‘security’ yenye ulinzi madhubutu ambayo ni ‘face id’. Kupitia ‘face id’ una uwezo wa kufungua simu yako haraka zaidi kwa kuitazamanisha sambamba na paji la uso. Lakini pia ina ‘fingerprint’ yenye kufungua simu yako kupitia alama za vidole.

  Pamoja ya kua kifaa hiki kinaendeshwa na Android 8.1 pamoja na processor ya 1.3Ghz quad core yenye kuipa simu kasi ya kufanya kazi kwa haraka zaidi na kupunguza uishaji wa chaji kwa haraka, lakini bado Spark 2 ina betri lenye ujazo wa 3500mAh. Kupitia Spark 2 unapata uhuru wa kusikiliza mziki, kupiga picha na kufanya kazi mbalimbali pasipo kikomo.

  Kwa wale wapenzi wa simu nzuri, hakika hiki ni kifaa kwa ajili yako.
  Last edited by TECNO SPOT TZ; 06-22-2018, 11:26 PM.

 • replied
  good

  Leave a comment:


 • replied
  jinsi ya kudowload pleas

  Leave a comment:


 • replied
  haina font changer ????

  Leave a comment:


 • commented on 's reply
  Tafadhali Hakikisha message center number ipo sawa

 • replied
  mbona kwangu received message azifiki kwangu tangu nilipo update version

  Leave a comment:


 • commented on 's reply
  Habari. Tumia aplikesheni ya File Go, hiyo ni kama file manager katika Spark 2

 • replied
  nimeinunua leo tecnospark2 Haina file Manager nitumieni

  Leave a comment:


 • commented on 's reply
  hatari sana sheikh wangu!

 • replied
  ni shida

  Leave a comment:


 • replied
  mh mh udalali hu

  Leave a comment:


 • replied
  jaman naitaji kufrash simu yangu tecno c8

  Leave a comment:


 • replied
  excellent job

  Leave a comment:


 • commented on 's reply
  bei elekezi ni 280,000/= TShs.

 • replied
  nic

  Leave a comment:

Advanced Options
Working...
X
Download the App for a More Fluid Experience
DOWNLOAD