This is a sticky topic.
X
X
 • Filter
 • Time
 • Show
Clear All
new posts

 • Jinsi ya Kupunguza Kujaa kwa Storage Space katika simu yako. Tanzania

  Inakuaje wadau!
  Ijumaa ndio hiyo inaishia.. hii inamaanisha kitu kimoja tu kwamba weekend inakuja.


  Sasa kama ilivyokawaida ya baadhi yetu kwenda mitoko mbalimbali weekend huku tukipiga picha tele na kuchukua video nyingi, leo nawaletea baadhi ya vitu tu ambavyo Unaweza kufanya ili kuzuia simu yako kujaa na kuishiwa nafasi ya kuhifadhi vitu vingine.

  Kabla ya kuanza kuelezea, tujue baadhi ya vitu ambavyo hua vinasababisha kujaza nafasi kwenye simu yako. Vitu hivyo ni kama vile mafaili ya video, picha au sauti kama vile nyimbo, applications, magemu, n.k.
  Na kama tunavyojua kua watu wengi tunatumia simu zenye storage space ya GB 8 au 16; hizi ni baadhi tu ya njia ambazo Unaweza kutumia ili kupunguza utumiaji mkubwa wa storage space katika simu yako.


  Baki na Application ambazo ulizikuta zimeshakua installed kwenye simu yako. Kwa kawaida simu hua zinakuja na applications muhimu ambazo zinakusaidia kufanya almost kila kitu. Ni vizuri kubaki kutumia hizo na kuinstall nyingine chache za ziada tu, na sio kuinstall applications nyingi ambazo zinafanya kitu kimoja.

  Tumia Cloud Storage. Hii na kama vile Google photos ambapo Unaweza hifadhi picha na videos zako on air na kuzifuta kwenye simu yako ambapo itakufanya simu yako isiweze kujaa. Pia Unaweza kutumia Google drive, one drive na cloud storage nyingine nyingi tu.

  Usidownload, bali stream. Kama kuna videos ambazo huoni ulazima wa kuzihifadhi kwenye simu yako, basi unaweza kuziangalia kwa kuzistream tu bila ya kuzidownload.

  Futa au Unistall applications ambazo hua huzitumii au ambazo unaona hazina umuhimu. Maana zitakua zinakaa tu na kufanya updates huku zikiwa zinakumalizia nafasi kwenye simu yako.

  Na hizo ni baadhi tu ya njia ambazo kwa harakaharaka Unaweza ukawa unazitumia kukusaidia kupunguza kasi ya simu yako kujaa haraka.
  Kama una njia nyingine yoyote Unaweza kuchangia pia.

  Weekend njema wadau!


 • #2
  gat u

  Comment


  • #3
   Originally posted by SedumaJr
   gat u
   high

   Comment


   • #4
    Thanks

    Comment


    • #5
     cloude storage inapatikana kipengele gani na hiyo stream naomba msaada

     Comment


     • waku7bisha commented
      Editing a comment
      Cloud storage ni storage apps kama vile Google Photos na Google Drive, Unaweza ukahifadhi vitu vyako huko na kuvifuta kwenye simu yako ili uweze pata nafasi.
      Kustream ni kama vile unavyoangalia YouTube videos pasipo kudownload

    • #6
     aje :0x1f637:

     Comment


     • #7
      clear cache of most apps in your phone

      Comment


      • #8
       kufuta thumbnails too

       Comment


       • waku7bisha commented
        Editing a comment
        Kweli kabisa. Ntaandika article ya jinsi ya kufanya hivyo ili watu waweze kuelewa.

      • #9
       Originally posted by socky
       cloude storage inapatikana kipengele gani na hiyo stream naomba msaada
       mm sim yangu imejaa hata sina vitu ving kwenye simu

       Comment


       • waku7bisha commented
        Editing a comment
        Jaribu kufanya vitu hivyo ambavyo vimependekezwa hapo juu

      • #10
       Originally posted by farrakhan jr
       kufuta thumbnails too
       ndio vitu gan ivo

       Comment


       • waku7bisha commented
        Editing a comment
        Thumbanails ni sehemu ambayo zinahifadhiwa picha na video ambazo umeshawahi zifungua na kuziangalia

      • #11
       Angejibiwa tungekua tumejibiwa wengi

       Comment


       • waku7bisha commented
        Editing a comment
        Habari.
        Una shida gani tuweze kukusaidia?

      • #12
       jamani Mimi sim yangu haitoi options za USB hata kama ukichomeka kwenye compta inakwambia your USB damage kwanini

       Comment


       • waku7bisha commented
        Editing a comment
        Habari.
        Tafadhali tutumie screenshot

      • #13
       naomben kujua jinsi ya setting ya memory card maana nimeweka lkn bado simu inaniambia internal full sasa hyo external nimeweka lkn bado msaada jaman

       Comment


       • waku7bisha commented
        Editing a comment
        Ukiweka memory card inabidi uende kwenye settings na kuiformat memory card kama internal storage

      • #14
       ?

       Comment


       • #15
        asante

        Comment

        Advanced Options
        Working...
        X
        Download the App for a More Fluid Experience
        DOWNLOAD