This is a sticky topic.
X
X
 • Filter
 • Time
 • Show
Clear All
new posts

 • Simu Ina Staki au ipo Slow? Fahamu ni kwanini, na jinsi ya Kutatua tatizo hilo. Tanzania

  Watu wengi wamekua wakiuliza juu la hili swala la kwanini simu zao zipo slow au zinastaki. Hata marafiki zangu pia wamekua wakiniuliza, nikaona leo tuliongelee kidogo swala hili.

  Nimejaribu kuchunguza na kupitiapitia baadhi ya blogs, kuwauliza baadhi ya watumiaji wa simu hizo, na mimi mwenyewe kujaribu baadhi ya vitu, nikapata vitu hivi baadhi ambavyo vinasababisha simu kua slow au kustaki.

  i/ Kua na kiasi kidogo cha RAM kwenye simu yako.
  Kufungua apps nyingi kwenye simu kama hiyo kunafanya baadhi ya apps kukosa nafasi na kufanya simu kustaki au kua slow.

  ii/ Kutumia Program zinazotumia internet kwa kasi
  Tuchukulie kwa mfano WhatsApp. Una magrupu mengi ya WhatsApp na yanatuma meseji mara kwa mara. Simu yako inalazimika kila mara kucheki kama kuna meseji mpya ili ikuletee notification. Kitendo hicho kinatumia kiasi cha RAM, sasa kama simu yako itakua na RAM ndogo, Tatizo ndio hapo linapoanza kutokea.

  iii/ Kutumia app ya Facebook
  Facebook ukishainstall na kufanyafanya updates, hua inachukua nafasi Zaidi ya MB 200 huko. Hii kwa wale ambao simu zetu zina nafasi ndogo za storage pamoja na RAM ndogo, inafanya simu inastaki na kua slow.

  iv/ Kutumia app ya Facebook Messenger
  Hii ni kama vile Facebook, ukishainstall na kufanyafanya updates, inakua inachukua kiasi kikubwa cha nafasi ya storage pamoja na RAM.

  v/ Kutozima simu mara kwa mara

  vi/ Kutofunga apps baada ya kumaliza kuzitumia
  Hapa watu wengi hua tunabonyeza tu ile button ya katikati (home button). Hiyo hua haifungi app moja kwa moja, inaiweka kwenye background ambapo RAM ndio hua inatumika kuhifadhi. Baada ya muda apps zikiwa nyingi, simu ndio inaanza kua slow au kustaki.

  vii/ Kutumia simu muda mrefu ikiwa na kava

  Jinsi ya Kutatua Tatizo
  - Kutumia Lite apps kama vile Facebook lite na Messenger lite.
  - Kua na utaratibu wa kuizima simu yako kwa muda mfupi mara tatu au nne kwa wiki
  - Zuia apps ambazo huzitumii kutuma notifications
  - Funga apps baada ya kumaliza kuzitumia.
  - Zima internet pale ambapo huitumii kabisa
  - Toa kava kama unatumia simu kwa muda mrefu.

  Ni hayo tu, kama kuna mengine tunaweza kuzidi kuelimishana chini hapo kwenye comments. Wale wenye simu zenye uwezo mdogo wa RAM na storage, ni muhimu kuzingatia hayo.
  Last edited by TECNO SPOT TZ; 09-07-2018, 05:52 PM.

 • #2
  Me simu yangu kila nikitoka kwenye whatsapp, facebook na baadhi ya application huwa zinaniandikia whatsapp is not responding, so naomba msaada wenu tafadhari

  Comment


  • waku7bisha commented
   Editing a comment
   Habari, pole sana kwa tatizo lako. Tafadhali Hakikisha simu yako haijajaa au haikaribii kujaa.
   Pia Hakikisha hua unaclear apps zote kwenye background.
   Kisha kwa kila application ambayo hua Inakuletea ujumbe hua, Fanya haya yafuatayo. Mfano kama ni WhatsApp;
   Nenda kwenye settings > apps > WhatsApp > Clear cache > Kisha restart simu yako.

 • #3
  Kava la simu linahusiana vp na simu kuwa slow !?

  Comment


  • waku7bisha commented
   Editing a comment
   Kwenye cooling process, kuna baadhi ys makava hua hayaruhusu joto kupita. Hivyo yanakua yanatrap (yanalundukiza) joto lote kwenye simu. Simu inapata moto, processor inapata moto na Kupunguza ufanisi wake wa kazi. Hivyo kusababisha simu kua slow au kustack

 • #4
  asante sana kwa Maelezo

  Comment


  • waku7bisha commented
   Editing a comment
   Karibu tena

 • #5
  good

  Comment


  • #6
   je Kama simu yangu ina tatizo LA kuniandikia isn't responding ya kila time inakuja kila Mda Mara file hili isn't responding nitatatuaje hili tatizo

   Comment


   • waku7bisha commented
    Editing a comment
    Nenda kwenye settings > apps > chagua hiyo app > clear cache > kisha reboot your device

  • #7
   Yaani Mimi hii simu hadi nimeichoka haina hata mwaka lakini inaweza kustuck hadi najuta bora hela yangu ningeiweka tu maana nazima kila siku usiku ndo kwanza limegoma hata touch na whatsApp na hiyo fb mnayosema tuache kutumia sa nini maana ya kuwa na smart

   Comment


   • waku7bisha commented
    Editing a comment
    Habari, pole sana kwa tatizo lako. Sio kwamba uache kutumia FB, ila utumie version ya Lite ya facebook, Facebook Lite.

  • #8
   yan cjakuelewa kbx

   Comment


   • #9
    my camera is not working pliz assist

    Comment


    • waku7bisha commented
     Editing a comment
     What error message are you getting?

   • #10
    hey. any?

    Comment


    • #11
     Umeelewekaaaaa kinoumaaa mkuu tena sana

     Comment


     • #12
      Simu yangu ina niletea ujumbe huu ''''Unfortunately, Shell has stopped"" mara kwa mara na pia nikiwasha data huwa inajiset kwenye silent mode msaada please kwa hili
      Last edited by roja; 09-15-2018, 07:15 PM. Reason: solution

      Comment


      • #13
       maelezo mazuri

       Comment


      • #14
       camera yangu haifanyi kazi msaada tafadhar

       Comment


       • waku7bisha commented
        Editing a comment
        Habari, pole sana kwa tatizo lako.
        Inakuletea ujumbe gani?

      • #15
       sawa

       Comment

       Advanced Options
       Working...
       X
       Download the App for a More Fluid Experience
       DOWNLOAD