This is a sticky topic.
X
X
 • Filter
 • Time
 • Show
Clear All
new posts

 • Simu Ina Staki au ipo Slow? Fahamu ni kwanini, na jinsi ya Kutatua tatizo hilo.

  Watu wengi wamekua wakiuliza juu la hili swala la kwanini simu zao zipo slow au zinastaki. Hata marafiki zangu pia wamekua wakiniuliza, nikaona leo tuliongelee kidogo swala hili.

  Nimejaribu kuchunguza na kupitiapitia baadhi ya blogs, kuwauliza baadhi ya watumiaji wa simu hizo, na mimi mwenyewe kujaribu baadhi ya vitu, nikapata vitu hivi baadhi ambavyo vinasababisha simu kua slow au kustaki.

  i/ Kua na kiasi kidogo cha RAM kwenye simu yako.
  Kufungua apps nyingi kwenye simu kama hiyo kunafanya baadhi ya apps kukosa nafasi na kufanya simu kustaki au kua slow.

  ii/ Kutumia Program zinazotumia internet kwa kasi
  Tuchukulie kwa mfano WhatsApp. Una magrupu mengi ya WhatsApp na yanatuma meseji mara kwa mara. Simu yako inalazimika kila mara kucheki kama kuna meseji mpya ili ikuletee notification. Kitendo hicho kinatumia kiasi cha RAM, sasa kama simu yako itakua na RAM ndogo, Tatizo ndio hapo linapoanza kutokea.

  iii/ Kutumia app ya Facebook
  Facebook ukishainstall na kufanyafanya updates, hua inachukua nafasi Zaidi ya MB 200 huko. Hii kwa wale ambao simu zetu zina nafasi ndogo za storage pamoja na RAM ndogo, inafanya simu inastaki na kua slow.

  iv/ Kutumia app ya Facebook Messenger
  Hii ni kama vile Facebook, ukishainstall na kufanyafanya updates, inakua inachukua kiasi kikubwa cha nafasi ya storage pamoja na RAM.

  v/ Kutozima simu mara kwa mara

  vi/ Kutofunga apps baada ya kumaliza kuzitumia
  Hapa watu wengi hua tunabonyeza tu ile button ya katikati (home button). Hiyo hua haifungi app moja kwa moja, inaiweka kwenye background ambapo RAM ndio hua inatumika kuhifadhi. Baada ya muda apps zikiwa nyingi, simu ndio inaanza kua slow au kustaki.

  vii/ Kutumia simu muda mrefu ikiwa na kava

  Jinsi ya Kutatua Tatizo
  - Kutumia Lite apps kama vile Facebook lite na Messenger lite.
  - Kua na utaratibu wa kuizima simu yako kwa muda mfupi mara tatu au nne kwa wiki
  - Zuia apps ambazo huzitumii kutuma notifications
  - Funga apps baada ya kumaliza kuzitumia.
  - Zima internet pale ambapo huitumii kabisa
  - Toa kava kama unatumia simu kwa muda mrefu.

  Ni hayo tu, kama kuna mengine tunaweza kuzidi kuelimishana chini hapo kwenye comments. Wale wenye simu zenye uwezo mdogo wa RAM na storage, ni muhimu kuzingatia hayo.
  Last edited by TECNO SPOT TZ; 09-07-2018, 05:52 PM.

 • replied
  Sorry mimi tangu juzi inagoma nikiingia instagram naambiwa can't refresh na whatsapp ndo siingii kabisa

  Leave a comment:


 • commented on 's reply
  inasumbua kivipi? nini shida? Inakuletea ujumbe gani? unakwama wapi?
  Tafadhali tuelezee tatizo lako vizuri Zaidi.

 • replied
  simu yangu inasumbua kutunza majina kwenye email yangu nifanyeje?

  Leave a comment:


 • commented on 's reply
  Tafadhali back up data zako na ufanye factory reset.

 • commented on 's reply
  TECNO wana simu za kila aina kulingana na bajeti yako na uwezo wa simu yenyewe. Kuna Low end, Mid end na high end smartphones. Sio kila simu zipo sawa kiuwezo

 • replied
  Originally posted by nyauba
  tecno k7 mbona slow sana
  baba sio poa k7 jau kinoma

  Leave a comment:


 • replied
  sim yangu kila Mara inakaa inaandika ujumbe unaosema unfortunately shell has stopped nifanye nini Ili kuziwia ujumbe huo?

  Leave a comment:


 • replied
  me ndo maana tecno zilinishinda maana simu zake unapangiwa matumizi kama iphone me nataka niwe huru kama nilivo na samsung yangu hapa naenjoy xana cwez tumia simu ya kujibana

  Leave a comment:


 • commented on 's reply
  Nenda kwenye app ya Phone master na useti ni app gani itumie na gani isitumie data on the background

 • replied
  Mm ninatumia mitandao ya kijamii,hivi mfano nataka kucheki mpira,na nahitaji kufunga app ili kupunguza utumiaji wa data,je ntafanyaje?

  Leave a comment:


 • replied
  Originally posted by Alexgeorge
  Me simu yangu kila nikitoka kwenye whatsapp, facebook na baadhi ya application huwa zinaniandikia whatsapp is not responding, so naomba msaada wenu tafadhari
  ?? Hili tatizo hata kwangu me ni ttzo hua nawaza ningekua na hela hiii simu ningeipigiza kwenye sakavu likawa vipande vipnde lkini ndyo hvyo sina kila kitu

  Leave a comment:


 • commented on 's reply
  Tafadhali back up data zako na ufanye factory reset..

 • commented on 's reply
  pa1 sana!

 • commented on 's reply
  Tafadhali back up data zako na ufanye factory reset.
Advanced Options
Working...
X
Download the App for a More Fluid Experience
DOWNLOAD