This is a sticky topic.
X
X
 • Filter
 • Time
 • Show
Clear All
new posts

 • HII NDIO SIMU MPYA YA TECNO PHANTOM 8 Tanzania

  Tecno tayari wameshatuletea Legendari wetu, Phantom 8, ambayo ilizinduliwa rasmi pale Jumeirah Hotel, Dubai. Phantom 8 ni kaka wa Phantom 6 na Phantom 6 plus ambazo ziliachiliwa hapo septemba 2016. Hiki kifaa ni hatari aysee, yaan imeonesha kua ni kali Zaidi ya wadogo zake. Ebhana ngoja nisipoteze muda wako, twende moja kwa moja kukifungua kifaa hiki kipya.

  ​Boksi la Phantom 8 lina nailoni hivi imelizunguka boksi ili kulilinda na vumbi pamoja na unyevunyevu. Nailoni wadau nilishalitoa tayari kabla sijaanza kuandika huu uzi sababu nilikua na mzuka wa kuiona Phantom 8.

  ​Boksi lake ni jeusi na sio kubwa kivile kama la Phantom 6 plus. Lina nembo ya Phantom 8 kila upande na namba nane inayong'aa hivi kwa juu.

  Click image for larger version

Name:	1.jpg
Views:	1
Size:	79.9 KB
ID:	12166  Baada ya kufungua boksi, unakutana na kitu cha Phantom 8 pale kimetulia vizurii katikati ya viboksi viwili vyenye mazagazaga yaliyokuja na Phantom 8
  Click image for larger version

Name:	2.jpg
Views:	1
Size:	122.7 KB
ID:	12167  Hakika hiki kifaa kimejitosheleza. Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo vimeambatana ndani ya boksi
  • Simu yenyewe ya Phantom 8
  • Kichwa cha chaji na waya wa USB Type C
  • Earphones
  • Kijitabu cha jinsi ya kutumia simu
  • Kava la simu (Sio la kufunga na kufungua, transparent)
  • Kipini cha kutolea line
  Click image for larger version

Name:	3.jpg
Views:	1
Size:	454.0 KB
ID:	12168

  ​Pia kuna zile documents hivi kama warranty card, kadi ya Boom play, ...
  Click image for larger version

Name:	4.jpg
Views:	1
Size:	112.5 KB
ID:	12169  Tecno pia wametuwekea kava la nyuma buree kabisa pamoja na screen protector
  Click image for larger version

Name:	5.jpg
Views:	1
Size:	471.6 KB
ID:	12170


  Fast charger kabambe kabisa na waya wa USB Type C

  Click image for larger version

Name:	6.jpg
Views:	1
Size:	410.8 KB
ID:	12171  Earphones maridhawa kabisa
  Click image for larger version

Name:	7.jpg
Views:	1
Size:	446.7 KB
ID:	12172  ​Tuachane na hizo accessories sasa, twende kukiangalia kifaa chenyewe kwa uzuri kabisa. Binafsi kitu cha kwanza ambacho kimenikosha ni hii mambo wenyewe wanaita 4GLTE worldwide roaming.
  ​Hii inamaanisha waweza tumia Phantom 8 popote pale duniani

  Click image for larger version

Name:	8.jpg
Views:	1
Size:	171.9 KB
ID:	12173  ​Kuna haka kaprotector transparent cha nailoni kwa mbele hv na nyuma ka kuzuia simu isipate scratch
  Click image for larger version

Name:	9.jpg
Views:	1
Size:	443.9 KB
ID:	12174

  Click image for larger version

Name:	10.jpg
Views:	1
Size:	467.3 KB
ID:	12175
  ​Kifaa chenyewe ni chepesi na kinashikika vizuri kabisa kutokana na 5.7 inch display iliyonayo
  Click image for larger version

Name:	11.jpg
Views:	1
Size:	412.3 KB
ID:	12176  Juu ya kioo kuna kamera ya kutwanga maselfi yenye 20 MP, spika kwa ajili ya calls na dual flash lights.
  Click image for larger version

Name:	12.jpg
Views:	1
Size:	329.2 KB
ID:	12177  Kwa nyuma sasa wamesimama malegendari wenyewe kamera mbili 13 MP & 12 MP Refocusing camera pamoja na tri Flash na fingerprint scanner.
  Click image for larger version

Name:	13.jpg
Views:	1
Size:	569.3 KB
ID:	12178  ​Kwa upande wa kulia wa simu kuna button ya power na zile za sauti.
  Click image for larger version

Name:	14.jpg
Views:	1
Size:	487.8 KB
ID:	12179  Sehemu ya kuwekea line ipo upande wa kushoto na unaweza kuitoa kwa kutumia kile kipini ambacho kimekuja na boksi tayari.
  ​Unaweza ukatumia line mbili zote kwa pamoja, au line moja na memory card. Huwezi kuweka line mbili na memory card kwa wakati mmoja

  Click image for larger version

Name:	15.jpg
Views:	1
Size:	436.2 KB
ID:	12180

  Click image for larger version

Name:	16.jpg
Views:	1
Size:	478.5 KB
ID:	12181  Kuna katundu cha kuchomeka earphone kwa juu kama ilivyo kwenye simu zingine za Tecno
  Click image for larger version

Name:	17.jpg
Views:	1
Size:	394.0 KB
ID:	12182  Spika, mistari ya antenna, mic na port ya kuchajia vyipo kwa chini
  Click image for larger version

Name:	18.jpg
Views:	1
Size:	428.7 KB
ID:	12183  Kuiwasha kwa mara ya kwanza pamoja na kuiseti ni rahisi sana kama vile kumsukuma mlevi. Phantom 8 imekuja na Android 7.0 Nougat pamoja na HIOS 3.0
  Click image for larger version

Name:	19.jpg
Views:	1
Size:	87.2 KB
ID:	12184  Kwa ujumla Phantom 8 ni kifaa cha ukweli kabisa kulingana na nilivyokiona na kukitumia kidogo kwa mara ya kwanza, ni dhahiri kabisa kua Tecno wamefanya kazi nzuri.

  Sifa za Phantom 8
  Name: Phantom 8
  Model : AX8
  Dimension : 159.95*79.5*7.9mm
  Processor: 2.6GHZ Octa-core
  Resolution : 1920*1080 Display : 5.7 FHD Touchscreen
  Memory : 64GB ROM + 6GB RAM Expandable Micro SD up to 2TB
  Camera Front : 20MP Front Camera with Dual flash.
  Camera Back: 12MP & 13MP AF Dual Back Camera with tri Flash.
  OS : Android 7.0™ with HIOS 3.0
  Network : GSM /WCDMA/ LTE
  Connectivity : GPS,WIFI, BT,USB Type C ,USB OTG.
  Battery Capacity: 3500 mAh
  Sensor: G-Sensor , Ambient Light Sensor, Proximity sensor , E-Compass, Gyroscope


  This post is the Courtesy of @Ennyholar
  Last edited by waku7bisha; 10-23-2017, 10:15 PM.

 • #2
  bei

  Comment


  • #3
   @waku7bisha,Well done,Give a thumbs up!

   Comment


   • waku7bisha commented
    Editing a comment
    Thank you

  • #4
   haitapungua 850,000 au itakuwa zaidi ya hapo.. maana bei ya dubai ni sawa na dinar 1,399 ambazo ni sawa na usd 380 <br />
   <br />
   Originally posted by Mauna
   bei

   Comment


   • #5
    Ni simu nzuri saana naomba kujua bei yake hapa tanzania tunaweza kupata kwenye maduka.yapi maalumu.

    Comment


    • #6
     simu iko puwa tupe location kwa dar inaptikana wapi

     Comment


     • #7
      the phone looks nice, we are still waiting to see, feel and if possible buy 1

      Comment


      • #8
       Iko poa sana bei ya hapa tz sh. Ngapi

       Comment


       • #9
        It looks nice. Tutasubiri kidogo before buying.. Phanthom 6 yangu ina miezi minne tu.

        Comment


        • #10
         so nice,bei yake vipi

         Comment


         • #11
          safi Kaibisa. nauza phantom 6+ naamia Phantom 8 nimeipenda hii

          Comment


          • #12
           tisha sana huyu ligendari

           Comment


           • #13
            Phantom 8 imenikonga Sana kwa kwa na Sensor za kutosha. hasa Ile ya Compass

            Comment


            • #14
             lini inatua bongo?

             Comment


             • #15
              inauzwa bei gani? na ni maduka gani? inapatikana simu hiyo

              Comment

              Advanced Options
              Working...
              X
              Download the App for a More Fluid Experience
              DOWNLOAD